Unaweza kufuta jumbe za sauti ambazo umetuma kwenye gumzo. Unaweza kuchagua kufuta ujumbe kwa ajili yako mwenyewe tu au kwa kila mtu kwenye gumzo.
Ukichagua Futa kwa Ajili Yangu wapokeaji bado wataona ujumbe wa sauti kwenye skrini yao ya gumzo. Hata hivyo, ukichagua Futa kwa Kila Mtu ujumbe wa sauti utaondolewa kwenye skrini ya gumzo ya kila mtu. Mara tu ujumbe wa sauti unapofutwa, hautaonekana tena kwenye gumzo.
- Fungua gumzo lenye ujumbe wa sauti unaotaka kufuta.
- Gusa na ushikilie jumbe za sauti.
- Gusa Futa > Gusa Futa kwa Kila Mtu au Futa kwa Ajili Yangu.