Kuhusu viungo vyenye shaka

Kwa baadhi ya viungo unavyopokea katika soga, unaweza kuona kiashirio cha kiungo kinachotiliwa shaka. Kiashirio hiki kinaweza kuonekana wakati kiungo kina mchanganyiko wa herufi ambazo huchukuliwa kuwa si za kawaida. Watumaji taka hutumia michanganyiko ya herufi ili kukuhadaa uguse viungo. Viungo hivi vinaweza kuonekana kwenda kwenye tovuti halali, lakini kwa kweli vinakupeleka kwenye tovuti hasidi.

Hapa kuna mfano wa kiungo kinachotiliwa shaka:
https://fåcecall.com/free-tickets

Kumbuka: Herufi ya kwanza inaonekana kama herufi "a" lakini badala yake ni herufi "å". Hii inamaanisha kuwa mtumaji taka anaweza kuwa amekuhadaa kutembelea tovuti ambayo haikuhusiana na FaceCall.

Unapopokea viungo, kagua kwa uangalifu maudhui ya ujumbe. Ikiwa kiungo kimewekwa alama ya kutiliwa shaka, unaweza kugonga kiungo na ujumbe ibukizi utaonekana. Ujumbe huo utaangazia herufi zozote zisizo za kawaida ndani ya kiungo. Kisha unaweza kuchagua kufungua kiungo au kurudi kwenye soga. FaceCall hufanya ukaguzi kiotomatiki ili kubaini ikiwa kiungo kinatiliwa shaka ili kulinda faragha yako. Kumbuka, kwa sababu ya usimbaji fiche wa mwisho hadi mwisho, FaceCall haiwezi kuona maudhui ya ujumbe wako.

More Resources

  • Support Team

    Reach our to our Support team for more help! Email us at support@facecall.com

  • Our Support Team is available:

    24/7/365

  • Follow us on Facebook!

    Get the latest news and updates first